Wednesday, July 1, 2020

WATU WASIOSHAURIKA

TAMBUA SIFA ZA WATU WASIOSHAURIKA
Wewe bila shaka ni mmoja kati ya watu ambao kuna tabia za ndugu,rafiki,mwajiri,mfanyakazi au yeyote unatamani aziache na haziachi na ulishajaribu kumpa ushauri na hashauriki na unakosa furaha kwasababu yake na hujui nini ufanye.

Leo nitakuorodheshea sifa za watu wasioshaurika.
Mtu asieshaurika anaweza kuwa yeyote msomi,asiekuwa msomi,kijana,mzee,mzazi au rafiki.

1.MTU ASIEKUBALI MAKOSA YAKE
wapo watu hawakubali makosa yao hata ukimkamata na ushahidi hakubali kosa.Shauri unavyoweza hutafanikiwa.

2.MTU MUONGEAJI SANA
huyu ni yule mwenye hasira za karibu na kitu kidogo ataongea sana kutwa nzima,huyu anaweza kuzusha ongemvi kidogo akalalamika sana na kuhadithia kila mtu.
Watu wenye tabia hizi ni wabishi wa hoja za wengine na ukiongea lolote anapinga hata kama hajui lolote.Ukichaa ni kupinga jambo ambalo hulijui ndani yake.

3.BLAME GIVER
Hawa ni wataalamu wa kulaumu wengine,mvua ikinyesha atalaumu,jua likiwaka atalaumu,lolote utasema atalaum.Ukimfanyia wema atatafuta dosari,ukimpigia simu atakulaumu kwa siku hukumtafuta awali,ukikaa kimya atalaumu kwa sababu hujamtafuta kwa vyovyote vile atakuwa anaona kasoro kwako.Watu hawa huwa akikwazana na mtu kazini anapeleka ugomvi kwa ndugu au wanafamilia yake kuwalaumu,kama biashara haina wateja atalaumu ndugu zake.chochote kinachomtokea atalaumu na watu hawa huwa na jazba sana,kauli zao ni kama vile utanambia nini umezaliwa nakuona,huwa wakali sana,wanaamini wakifa hakuna wa kuziba pengo,huwa wanapenda wakudhalilishe mbele za watu,wanakukejeli mbele za watu,huwa hawatunzi siri,huwa wanakusema vibaya watu hawa shauri mpaka utoke povu hawashauriki.

4.MJUAJI SANA
Hawa wanajua kila kitu ukianzisha mada atadakia kabla hujaimaliza ataongea anachojua,wasiokusikiliza ,mtu anaetumia simu ukianza kuongea,mtu anaetaka kukutawala huwezi kumshauri,mtu anaekutabiribia mabaya huwezi kumshauri,mtu anaeamini anajua kila kitu,mtu ambaye ukiongea anatafuta dosari akukosoe badala  ya kuzingatia ujumbe,mtu mwenye hasira sana,mtu anehoji kwa jazba,mtu anaetumia silaha kwenye mabishano huwa hawashauriki,mtu anaekudharau huwezi kumshauri,mtu aneamini hujui huwezi kumshauri,mtu mwenye kiburi huwezj kumshauri.

5.CHRONIC GOSSIP
Huyu ni mbea sana,ukimwambia jambo utalisikia kwa majirani huwezi kumshauri,mtu mwenye kupigana mafumbo au vijembe huwezi kumshauri.
Watu ambao unaogopa kuwatania kwa kuhofia watapokeaje utani huo huwezi kuwapa ushauri.

Kupata kitabu cha MALEZI YA UBONGO KISAYANSI na MISINGI 10 YA FURAHA SIKU ZOTE

+255766862579
+255622414991

Imeandikwa Na Psychologist
Said Kasege
Temeke,Dar es salaam

No comments:

Post a Comment