MOTISHA :MOTISHA SEHEMU YA 2
Tupo kwenye ulimwengu wenye matatizo mengi sana na suluhu za matatizo zipo ila wachache wanazijua.
Hakuna mtu asiekuwa na matatizo hata kama ataonekana kwenye mitandao akitabasamu kamwe usitamani maisha yake.
Kila mtu ni shahidi wa nafsi yake.Hakuna asiehitaji kufika hatua moja mbele au zaidi.
Kama unahitaji usogee walau hatua moja bila shaka kipo kitu kimekuzuia kufika hapo unapotaka ndio sababu kila mtu anahitaji motisha.
Kama mtu hajui anataka nini ndio njia yeyote ataenda.
Maumivu ni sehemu ya maisha ya binadamu.
Kila unaemuona amefanikiwa siku moja alikuwa kama wewe au chini zaidi yako.
Tofauti ni kwamba hawajakata tamaa.Lazima utakataliwa hata uweje lazima baadhi ya watu watakukatalia maombi yako.Hata uwe mzuri kiasi gani wapo watu wataona ubaya wako hata ufanyeje.
Hata uwe na huruma vipi wapo watu watasema unaroho mbaya.
Hata uwapende watu wote duniani wapo watu watakuchukia kisirisiri au kwa wazi.
Haijalishi unamaadui kiasi gani,hainalishi huna "connections",haijalishi huna pesa ya kula,haijalishi umepata ajali,haijalishi unafedheheka,haijalishi unamagonjwa sugu miaka nenda rudi huponi,haijalishi biashara zako haziingizi faida,haijalishi unafanyiwa figisu ufukuzwe kazi,haijalishi umetelekezwa na baba yako au mama yako,haijalishi kwenu hakuna mwenye kukusaidia,haijalishi kazi zote ulizotuma maombi umekataliwa,haijalishi umekosa mkopo wa masomo,haijalishi unalala chini,haijalishi hujasoma,haijalishi unatoka wapi jambo muhimu upo hai.
Haijalishi huna mtoto miaka nenda rudi,haijalishi unateswa na mama mkwe ,haijalishi ndugu wa mke au mume wanakuchukia na figisu wanakufanyia bado upo hai unaweza kufanya mabadiliko ya maisha yako.
Kamwe usikate tamaa.Kukata tamaa ndjo utakuwa umekubali kupoteza ushindi.
Kamwe usirudi nyuma.
Wapo watakukatisha tamaa ziba masikio.
Haijalishi kazi yako ni dhalili,haijalishi kazi yako kipato kidogo,haijalishi kazi yako unanyanyaswa,haijalishi kazi yako haina faida kubwa kwa sababu tu inakupa chakula basi inuka songambele.
Haijalishi ajira wanapata wengine we unakosa,haaijalishi umeachwa kwa kukksa pesa bado upo hai,inuka sogea hatua.
Sogea hata hatua moja hata kama huoni matokeo sogea,sogea,sogea utafanikiwa hata kwa kuchelewa.
Usimue roho kwa kuona wengine wanapata pesa kukuzidi,usiumie kuona wengine mambo yao yanaenda wewe hayaendi kama hnavyotarajia sogea hatua moja.
Kama watu wote wamekugeuka wewe sogea hatua moja,sogea,inuka,inuka tena,inuka tena mpaka ufike kwenye lengo.
Hata kama matokeo ni dhaifu sogea,sogea,hata kama maumivu ni makali sana sogea hatua moja,kamwe usikate tamaa hata kama watu wote wamekata tamaa juu yako wewe usikate tamaa.
Kupata kitabu cha MOTIVATION chenye jina BADILI FIKRA ZAKO BADILI MAISHA YAKO
Simu
+255766862579
+255622414991
Imeandikwa na Psychologist
Said Kasege
Temeke,Dar es salaam
No comments:
Post a Comment