Wednesday, July 1, 2020
JE UNAWEZA KUMPONGEZA RAFIKI YAKO AKIKUZIDI KIPATO? Katika vitu huwanyima watu wengi raha ni pale akimwona mtu anaemjua au aliezaliwa nae sehemu moja au kusoma nae pamoja akiwa na muonekano mzuri kumzidi. Watu wengi huwa wanafurahi akiona wale alisoma nao au kuzaliwa nao mwaka mmoja anawazidi kipato na kama akiona wanamzidi anajenga chuki au wivu. Kisaikolojia kutokana na kuongezeka kwa matumizi ya mitandao ya kijamii hasa facebook,instagram kumefanya watu wengi kuishi kwa kushindana. Mtu hata kama amelala njaa ataweka picha ya miaka sita iliyopita ikimwonesha anakula chakula kizuri,kama akiwa na marafiki zake ataweka picha kuonesha anapendwa sana,kama akitembelea sehemu atahakikisha watu wote wamejua kama amesafiri,kama anafanya tukio lolote atahakikisha watu wote wanajua. Kwa muktadha huo imepelekea baadhi ya watu kuwajengea chuki ndugu zao au marafiki kwa kuamini wanawazidi kipato. Kisaikolojia watu wenye kujilinganisha na wengine ndio hupata Depression,stress na kuchanganyikiwa hasa anapotaka maisha ya watu wengine. Kwenye mitandao ya kijamii watu wengi huonesha maisha yenye mafanikio ili kuhakikisha anakuwa mwenye kusifika kulkko mwengine. Kitendo cha mtu kutaka kuonekana yupo juu kuliko wengine kinasababishwa na low self-esteem. Tatizo la low self-esteem hupelekea ushindani usiokuwa na maana.Mtu mwenye furaha huwa hashindani na watu wengine bali anashindana na yeye mwenyewe kuhakikisha leo yake ni bora kuliko jana. Ni kawaida watu wengi wakiona picha kwenye mitandao ya kijamii kutamani maisha ya wengine kwa kuona wao ni bora kumzidi. Katika utafiti uliofanywa nchini Marekani ilibainika kuwa watu wengi hufanya uigizaji (fake life) kwenye mitandao ya kijamii. Yupo mwanamitindo alikuwa analazimika kupiga picha akiwa na nguo za bei ghali sana,akiwa sehemu za kifahari si kwamba ndio maisha yake halisi bali alikuwa akitangaza biashara za watu. Alieleza kuwa aliamua kuacha kwa sababu anaishi maisha fake na kipato chake. Hali inakuwa mbaya zaidi kwa watu wa kipato cha chini ambao huwa wanaamini kila picha ya mtandaoni huku wakitamani maish ya wengine kuliko wao. Kisaikolojia hakuna binadamu mwenye sherehe kila siku. Kama unasumbuliwa na stress za ajira wengine wanazo pia za afya,uzazi,kusengenywa,kuteswa,kubaguliwa,hasara kwenye biashara,kufiwa ndugu zao,kuingia madeni,kufeli masomo,kufukuzwa kazi,kufeli usaili,kupoteza mali kwenye mikopo n.k kwa vyovyote usitamani maisha ya wengine kama ukijua maisha yao halisi na matatizo wanayopitia utafurahia maisha yako. Wewe mwenyewe ni shahidi wa matatizo unayopitia na kama utasema huna tatizo linalokukabili bila shaka wewe ndio tatizo lenyewe. Kamwe usidhani wengine wanafuraha kila siku bila huzuni si kweli. Kila mtu anamatatizo yake. Ndio sababu unatakiwa furaha yako ujipe mwenyewe. Kama hakuna anaekupenda jipende wewe Kama hakuna anaekuamini jiamini wewe. Utabaini kuwa hakuna binadamu utadumu nae siku zote. Kamwe usiweke mafanikio yako kwenye maamuzi ya mtu mwengine. Chanzo cha furaha yako ni wewe mwenyewe. Unaweza jitazama kwenye kioo kisha ukatamani sura yako baadhi ya viungo angepewa mwengine kama unafikra hizo unasumbuliwa na Low self-esteem Watu maarufu hawana sura za ajabu kuliko wewe isipokuwa wamejiamini na kupiga kazi kwa ubora wa hali ya juu bila kujali kasoro ambazo hawawezi kuzibadilisha. Watu wasiojiamini hutumia cosmetics,vyakula,mavazi kubadili muonekano ili wawavutie watu wasiowapenda. Mtu mwenye kukupenda hahitaji ujibadilishe bali anakupenda vile ulivyo. Kupata kitabu cha MALEZI YA UBONGO KISAYANSI NA MISINGI 10 YA FURAHA SIKU ZOTE.Piga +255766862579 +255622414991 Imeandikwa na Psychologist Said Kasege Temeke,Dar es salaam
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment