Wednesday, July 1, 2020

KUKATA TAMAA

MAUMIVU YA KUKATALIWA NA KUFELI
Hakuna mtu hajakataliwa na hakuna mtu hajafeli.
Wapo watu hujisifu kuwa hawajawahi kufeli na hupenda watu wawasifie kwa kufanya kwao vitu bila kufeli.

Kuna aina 2 za watu Introvert na Extrovert.
Introvert ni wapole,wenye upendo sana wanafikiri kwanza kisha wanaongea,wanahuruma sana,hawana hasira,hawakati tamaa haraka,hawapendi makuu,huwa wavumbuzi wa vitu vyao wenyewe,hufurahia upweke.

Extrovert hawa ndio wengi duniani ambao sifa zao ni kama kuongea kwanza kisha wanafikiria,wanapenda sana mikusanyiko,hupenda show off,huwa wanapata furaha kwa vitu au watu wengine ,hawawezi kudhibiti hasira zao,huwa waongeaji sana,huwa wanapenda makuu.

Watu wapole wakifeli hawakati tamaa ila wenye hasira hukata tamaa haraka.
Watu wapole hawana makuu kama kupelekesha wafanyakazi,kudhalilisha wenza wao,huwa na mapenzi ya dhati,huwa wanatunza siri,huwa wagumu kuanzosha uhusiano kwa sababu huwa hawaamini watu kirahisi,huwa wanaweza kucheza na watoto kwa urahisi huku wakali wakiwa wanapenda kutawala wengine,hupenda kubadili tabia za wengine,hupenda visasi,mafumbo,kejeli.

Maumivu ya kukataliwa ni sawa na maumivu ya kupigwa na kitu mwilini.Ukifeli au kukataliwa unaweza kupata hasira sana na mtu akipata hasira kwa kufeli au kukataliwa huwa akili haifanyi kazi na maamuzi yoyote mtu akifanya kwa hasira ni mabovo na hupelekea tatizo kuliko suluhu.

Ukifeli au kukataliwa si dhambi bali tafuta njia mpya ya kujaribu,jaribu tena,tena,tena mpaka ufanikiwe usiangalie umefeli mara ngapi angalia mara ngapi hujafanya.

Watu wenye hasira za karibu hawawezi kujaribu mara nyingi zaidi wakifeli kwa sababu hupenda mafanikio ya kulala na kuamka.Watu wenye hasira huwa wanazijua njia nyingi zitakazofanya ufeli kuliko njia moja itakayo kufanya ufaulu.

Ukiwa na watu waliokata tamaa kisha ukataka wakupe ushauri watakukatisha tamaa kwa sababu wao wenyewe wamekata tamaa.

Watu wapole hawalipi kisasi.Watu wenye hasira wanaweza kumhukumu mtu kwa taarifa za kusikia bila uchunguzi.
Wangapi wanawachukia watu maarufu ambao hawajawahi hata kuwaona?
Jibu ni wengi kwa sababu wao kila taarifa wakipewa wanaamini hata uchunguzi hawafanyi.

Watu wenye hasira hawajifunzi kwa sababu huwa wanapinga hoja hata kama hawajui lolote juu ya hoja hio.

Watu wapole huwa wanauliza sana maswali ili wajifunze huku wenye hasira huuliza ili wakuoneshe wanajua kukuzidi.

Hasira zinaweza kuzuia mafanikio yako kwa kiwango kikubwa.

85% ya mafanikio yako yanatokana na tabia zako huku 15% ni ujuzi uliosomea.
Mtu akiwa na kiburi kwa sababu amesoma maana yake anajivunia 15% halafu kwenye tabia anakuwa amefeli.

Watu hawapendi kuishi na wenye kiburi kwa sababu kila binadamu hupenda aoneshwe upendo ni ngumu sana mtu mwenye kiburi kuwapenda wengine.

Ukikataliwa kwako ni fursa ya kukubaliwa kwengine.Kama umepoteza fursa nyingi sana amini fursa zingine nzuri zipo njiani kwa ajili yako.
Ukikataliwa na mtu wa kwanza nenda kwa mwengine,mwengine,mwengine usiangalie wangapi wamekukatalia utakata tamaa bali angalia wangapi hujawafuata.

Dunia hii ina watu bilion 7.8 huwezi kumkosa mtu mwenye fikra kama zako.
Watu wenye kukupa msaada huchelewa kuja kwa sababu hio ndio maana unahusiwa uvumilivu na kutokata tamaa.

Watu hukata tamaa kwa kukosa uvumilivu.Watu wanakosa uvumilivu kwa sababu ya hasira,watu wanahasira kwa sababu wanataka mafanikio ya kulala na kuamka.

Usiweke mafanikio ya kulala na kuamka utakata tamaa.

Watu wanakukatalia si kwa sababu wewe ni mbaya au wanakuchukia hapana wanakukataa kwa sababu zao wenyewe.

Kamwe usifikiri watu watakupenda kwa sababu zako lah watu wanakupenda kwa sababu zao wenyewe na wanakuchukia kwa sababu zao wenyewe.

Jiamini tambua kabisa huwezi kufanikiwa bila kufeli au kukataliwa.
Acha wakukatae,kubali matokeo hata kama mabaya anza upya nafasi unayo sababu tu upo hai kila kitu kitaenda vema.

Kupata kitabu cha
MALEZI YA UBONGO KISAYANSI NA
MISINGI 10 YA FURAHA SIKU ZOTE

+255766862579
+255622414991

Imeandikwa na Psychologist
Said Kasege
Temeke,Dar es salaam

No comments:

Post a Comment