LAWAMA HUMFANYA MTU ASIJIREKEBISHE
Katika maisha tunayoishi watu wengi huwa wanatupa lawama kwa wengine kama matokeo yakija tofauti.
Hasa wenye mamlaka kama mzazi kwa mtoto,mwajiri kwa mwajiriwa n.k huwa wakifanya hivyo na badala ya mtu kukiri kosa huwa anajitetea sana na kuacha dosari kama ilivyokuwa.
Ikiwa umewahi kushuhudia matukio mbalimbali kutoka katika maisha ya kila siku utakuwa umeona hali hiyo.
Kuna mfano wa mhandisi mmoja alikuwa anasimamia ujenzi eneo fulani ambapo vibarua walipewa kofia za ngumu za kujilinda dhidi ya vitu vikidondoka ili visiwadhuru.
Alikuja ghafla eneo la ujenzi akakutana na baadhi ya wafanyakazi hawajavaa kofia ngumu aliwafokea sana kwa tukio hilo.
Wakati anawafokea walivaa kofia zile huku walimsikiliza.
Alipomaliza kuwatofokea,kuwalaumu,kuwatishia aliondoka, ghafla vibarua wote walivua zile kofia hata wale waliokuwa wamevaa kwaa hiyari walizivua kwa hasira
Waliamua kuzivua kwa sababu waliona wanapelekeshwa pamoja na kuwa ni kwa faida yao ila waliamua kufanya jeuri kwa kuona wanamkomoa.
Hali hiyo ipo kila sehemu.Mke akiunguza chakula na mume akianza kufoka,kutukana,kulaumu,kumtishia huwa anachochea kiburi kwa mke na mke hawezi kujirekebisha kwa kosa hilo badala yake atajitetea kuwa hakuwa na njia tofauti zaidi ya hiyo.
Na kwa sababu kiburi huwa kinakuja mtu akifokewa inapelekea akatae kosa badala yake ataweka visingizio kibao vya kufanya kosa husika .
Mtu huongozwa na mihemko ambapo akiwa mwenye hasira hufanya jeuri sana na akiwa mwenye furaha sana hufanya mambo ya ajabu ila akili ikiwa imetulia anafanya maamuzi mazuri.
Hata wewe ukifokewa,kutukanwa,kulaumiwa,kutishiwa huwezi kufanya kazi kwa weledi utafanya liwalo na liwe hata kumkomoa utafanya ikibidi.
Mfano mwajiri akimtukana mfanyakazi mbele ya wafanyakazi wengine kwa akili ya mwajiri atajua ametoa onyo kumbe karipio hilo limewaumiza walioshuhudia wote ambapo kila mmoja atakuwa anahofu siku ikiwa zamu yake.
Hofu hiyo itafanya wafanyakazi kufanya kazi kwa kufuata maagizo tu ili wasimuudhi mwajiri kwa kuepuka kutolewa,kutukanwa,kuvuliwa wadhifa katika ofisi.
Kila mtu anakuwa na hofu ya kuanzisha jambo ambalo mwajiri atakuwa hajalipitisha hivyo kukosekana kwa ubunifu kwenye ofisi.
Mtoto huwa anafurahi sana anapoonyeshwa tabasamu kutoka kwa mzazi wake ambapo humfanya ampende sana mzazi wake kupita kiasi.
Mtoto akifokewa,kutukanwa,kutishiwa,kupigwa,kudhalilishwa kwa kauli za ubaguzi wa rangi,kabila,lafudhi,muonekano,ufaulu duni au kukosea mara kwa mara humfanya mtoto kumuogopa mzazi na huwa anakuwa mzito sana kushirikiana na wengine kwa hofu ya kukosea.
Mtoto huanza kujibagua kwa rangi,lafudhi,kabila,muonekano,ufaulu kwa sababu amesikia kauli hizo mara kwa mara.
Mtoto akisifiwa sana kuwa yeye ni mzuri sana,mwenye akili sana,mcheshi sana,mwerevu sana huwa anajichukulia tofauti na watoto wanaoteswa
Mtoto anaepewa pongezi kwa kazi nzuri anazofanya,kupewa zawadi kwa juhudi,kuahidiwa kufanyiwa mambo mazuri akifanya vizuri huwa mwenye juhudi kuhakikisha anamfurahisha mzazi wake kwa kuongeza juhudi katika kazi zake.
Mtoto anakatishwa tamaa,kukosolewa sana,kufokewa sana,kulaumiwa,kutuhumiwa uhalifu hata kama hajakosea huwa anakuwa mwenye hasira za kila wakati ambapo huwa hashauriki akiwa mkubwa kwa sababu kumchukulia kila mwenye mawazo tofauti kama adui kwa sababu tangu mtoto kila wazo lake lilipingwa vikali.
Mtu ambaye hawezi kupongeza juhudi za wafanyakazi waliopo chini yake huwa anafanya hivyo kwa sababu ya chuki,wivu,kisirani, kuhisi atapokonywaa cheo kama anayefanya vizuri atakubalika sana kumzidi.
Wapo watu kwenye ofisi akifika wafanyakazi huanza kujifanya wapo busy ili wasidhalilishwe mbele za wageni
Ambao ni waajiri wenye uelewa huwa inakuwa rahisi kupewa ushirikiano kutoka kwa watu waliopo chini yake huku yule mwajiri mwingi wa lawama kila mtu humkimbia
Ukiona wafanyakazi wenzio hawakuonyeshi ushirikiano ujue wewe ndiyo tatizo.
Kama unawatukana,kuwadhalilisha, kuwalaumu sana,hutoi pongezi mtu hata akifanya kazi nzuri kiasi gani,unakosoa kila juhudi za wafanyakazi,kuwaamini hata wafanyeje utaona hawakuonyeshi ushirikiano.
Kama unavyoona mtoto anapenda kupongezwa,kusifiwa,kupewa maneno laini hivyohivyo hata kwa watu wazima
Mke alipopewa maneno laini,asiposifiwa kwa muonekano wake,upishi,juhudi,tabia zake huwa anajiona kama hayupo sehemu sahihi na huwa mwenye hasira sana utasikia 'mimi sina jema humu ndani kila ninapofanya kazi zozote lazima zitakosolewa na lawama juu'
Kama ni kazini mfanyakazi huongeza juhudi kama anasifiwa kwa kazi anazofanya kwa sababu binadamu atafanya juhudi ila asipopewa pongezi huanza kujitilia shaka kuhusu kazi zake anajiuliza kama anafanya kwa usahihi au anakosea.
Mtu unapomlaumu unafanya awe na kiburi,hasira,chuki,kisasi,wivu,kuweka vinyongo,kuanza kusengenya
Hasira huwa inakuja kwa kila mtu hasa anapolaumiwa,kufokewa,kutukanwa,kudhalilishwa.
Wengine utasikia 'hivi kweli wewe umesoma? Chuo gani umesoma ambapo mnafundishwa ujinga kama huu?'
Hapo mtu huanza kupata hasira kwa sababu anaonekana hajasoma hata kama amesoma,kingine anajiona hafai,anajidharau,anapata hasira,anapata wivu,hasahau kauli hizo na huweza kubeba chuki na kutaka kulipa kisasi.
Wapo waliojiua kwa kukosolewa sana.
Kama wewe ni mtaalamu unapokosoa kazi zozote za watu tambua unaumiza hisia za watu hasa watu dhaifu ambao huamini uzuri wa kazi zao unatokana na maoni ya watu wengine.
Watu wanaojitambua huwa hawajali sana kauli mbaya za watu juu yao ila wengi ni dhaifu ambapo ukimkosoa tu tayari anaacha kile anachokifanya kwa hasira
Mfano mtu anampelekea zawadi mama yake mzazi lakini mama yake mzazi hana shukurani badala mzazi ampongeza mwanae kwa zawadi ataanza kuikosoa sana zawadi hiyo jambo hilo humfanya mtoto kujichukia sana na ikiwa mzazi atasifia zawadi ya mtoto mwengine atafanya chuki kuenea baina ya watoto wake kwa kuanza kuonana kama maadui japo ni tumbo moja.
Wapo wazazi hubagua zawadi za watoto ambapo mtoto mmoja akimpa zawadi atasifia na mwengine ataikosoa sana hata kama ni nzuri.
Kwa sababu binadamu huongozwa kwa hisia hufanya mgawanyiko kwa watoto ambapo huanza kuchukiana wao kwa wao
Hakikisha unajipenda sana hasa pale hakuna anaekuenda.
Jiamini sana hasa unapokosa mtu wa kukuamini
Jijali sana hasa pale unapokosa mtu wa kukujali.
Tabasamu hata kama moyo wako unavuja damu.
Kupata kitabu cha
1.FIKRA ZAKO FURAHA YAKO (softcopy)
2TIBA YA MSONGO WA MAWAZO (hardcopy & softcopy)
3.BADILI FIKRA ZAKO BADILI MAISHA YAKO (hardcopy & Softcopy)
4.MALEZI YA UBONGO KISAYANSI( hardcopy & softcopy)
5.TABIA ZA WATU WALIOFANIKIWA (Hardcopy & softcopy)
6 MISINGI 10 YA FURAHA SIKU ZOTE (hardcopy &softcopy)
+255766862579
+255622414991
Imeandikwa na Psychologist
Said Kasege
Temeke,Dar es salaam
